Wafungwa zaidi ya 900 watoroka gerezani Congo DRC

495
0
Share:

Zaidi ya wafungwa 900 wametoroka katika moja ya gereza nchini Congo DRC baada ya watu wasiojulikana kuvamia gereza hilo na kufanya shambulio lililosababisha vifo vya watu 11.

Katika tukio hilo watu hao walivamia na kuanza kurushiana risasi na askari waliokuwa wanalinda na wakati wakiendelea kurishiana risasi wafungwa hao walikimbia huku wafungwa wachache ndiyo wakibakia gerezani.

“Wafungwa kwenye gereza la Kangwayi lililopo Beni walivamiwa saa 9:30 mchana na watu ambao bado hawajajulikana,

“Kwa sasa kuna wafungwa 966 ambao wametoroka, na waliobaki ni gerezani ni 30 tu,” alisema gavana wa Kivu Kaskazini, Julien Paluku na kuongeza kuwa.

“Wakati tukio la kurushiana risasi kati ya watu wa usalama na washambuliaji, ilibainika kuwa kuna watu 11 wamefariki na kati yao nane ni maafisa wa usalama.”

Share:

Leave a reply