Wahalifu 13 wauawa na Polisi Kibiti, watelekeza Pikipiki mbili na silaha nane

417
0
Share:

Jeshi la Polisi limewaua wahalifu 13 katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti ambapo jumla ya silaha 8 aina ya SMG, risasi 158, pikipiki 2, pamoja na begi la nguo vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu hao vilipatikana.Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akielezea baadhi ya vitu mbalimbali vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu 13 waliouawa katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti ambapo jumla ya silaha 8 aina ya SMG, risasi 158, pikipiki 2, pamoja na begi la nguo vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu hao. Kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai (CP) Robert Boaz.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Chini ni silaha 8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo. 

Share:

Leave a reply