Wahapahapa Band wapagawisha tamasha la Sauti za Busara 2017

465
0
Share:

Tamasha la Sauti za Busara msimu wa 14 limeanza mchana wa jana 9 Februari 2017 huku tukishuhudia vikundi mbalimbali vya Burudani  kutoka ndani na nje ya Tanzania ambapo viliweza kutoa burudani ya aina yake.

Jioni burudani hiyo iliamia ndani ya viunga vya Ngome Kongwe ambapo majukwaa mawili ya burudani  yaliyosheheni vifaa  vya kisasa vya muziki Kimataifa.  Jukwaa la Amphitheatre na jukwaa kuu la Mambo Club

Vikundi 9 vya burudani viliweza kukonga nyoyo watu mbalimbali kutoka mataifa tofauti ambao kwa nyakati zote walijawa na mzuka kutoka jukwaani.

WAHAPAHAPA BAND

Kundi la Wahapahapa liliweza kupagawisha vilivyo katika jukwaa kuu na nyimbo zao mbalimbali  zikiwemo nyimbo za  “Kipanga”, “Alli Jojo”, “Cha bure”, “Dunia”, “Mapanya” na “Athumani/ Anamung’unyula”.

Mpaka sasa bendi hiyo imetimiza miaka 10, tangu  kuanzishwa kwake hapa nchini huku ikiwa imesheheni wasanii wenye ujuzi wa hali ya juu katika masuala ya muziki wa aina mbalimbali ikiwemo utamaduni

Bendi ya Wahapahapa wakitoa  burudani kwenye tamasha la Sauti za Busara 2017, usiku wa 9 Februari. 

Kiongozi wa bendi ya Wahapahapa akiwajibika kwenye jukwaa la Sauti za Busara 2017

Baadhi ya wanakundi wa bendi ya Wahapahapa wakiwa katika mahojiano maalum na wanahabari

Mahojiano na wanahabari yakiendelea

Kiongozi wa bendi ya Wahapahapa, Msanii Paul Ndunguru akielezea namna bendi hiyo inavyofanya shughuli zake mpaka sasa kufikia miaka 10 ya toka kuanzishwa kwake,amezungumza hayo muda mfupi baada ya kumalizika kwa shoo yao katika jukwaa la Tamasha la 14 la Sauti za Busara 2017. Picha zote na Andrew Chale.MO BLOG-Zanzibar

Share:

Leave a reply