“Wajiandae”- Ujumbe wa Spika Ndugai kwa mawaziri wapya

217
0
Share:
Job Ndugai

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo Oktoba 9, 2017 amewapongeza Mawaziri na Manaibu Waziri wapya walioapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam, na kuwataka wajiandae kwa ajili ya kufanya kazi.

Ndugai ametoa kauli hiyo baada ya mawaziri hao kuapishwa mbele ya Rais John Magufuli. 

“Napenda kuwapongeza wabunge ambao leo wamepata nyadhifa za kuwa mawaziri wa wizara mbalimbali na manaibu waziri maana ninyi mnatokana miongoni mwetu na Rais ameona awape majukumu ya kuongoza nafasi. Hao walioapishwa na waliokuwepo wajiandae tukienda Dodoma ni kazi tu, karibuni Bungeni Dodoma,” amesema na kuongeza. 

 “Nimkaribishe Katibu wa Bunge mpya Mgaimgai, katibu anayemaliza muda wake kumshukulu Kashilila ahsante sana kwa utumishi uliotukuka. ni matumaini ya watanzania kwamba timu hii inayohimarisha baraza la mawaziri na kuanza kazi le oleo kwenye kiikao cha Baraza la Mawaziri.”

Kwa upande wake Jaji Mkuu nchini, Profesa Ibrahim Juma amewataka kufuata katiba na sheria ili kusiwepo mgongano. 

“Nawapongeza mawaziri na manaibu na kuwatakia kila la kheri katika kazi, cha muhimu ni kufanya kazi, kwa upande wa mahakama tunaomba tufuate sheria, taratibu na katiba ya nchi, hakutakuwa na mgongano wowote,” amesema.

Mawaziri na Manaibu Waziri waliopishwa leo ni wale waliobadilishiwa wizara na wapya,akiwemo Waziri wa Tamisemi Selemani Jafo ambaye awali alikuwa Naibu Waziri, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Mkuchika , na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina aliyekuwa Naibu Waziri Mazingira na Muungano.

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply