Wakala wa Taifa wa Utafiti wa nyumba na vifaa (NHBRA) wabaini hewa ukaa kwenye majumba

231
0
Share:

Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya Ujenzi (NHBRA)  wameanza utafiti wa awali juu kiasi cha nishati  kinachotumika katika  shughuli za ujenzi pamoja na michakato yote ya kuandaa vifaa hivyo ikiemo utengenezaji, uchimbaji, usafirishaji ambapo utaafiti huo una lengo la kupunguza  kiwango cha hewa ya ukaa (greenhouse gases) kinachotolewa kwenye shughuli za ujenzi hivyo kupunguza uharibifu wa mazingira.

Wakizungumza mbele ya wanahabari, Mkandarasi wa NHBRA,  Muhandisi Benedict Chilla ameeleza kuwa kuwa wameweza kufikia mikoa minne na vijiji kadhaa katika mikoa hiyo ambapo wamebaini mambo mbalimbali wanayoendelea kuyafanyia utafiti ambapo miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na hewa ukaa ambayo ni hatari.

“Katika utafiti huu ambao ni awali tumetumia mwaka mmoja na miezi mitatu. Miongoni mwa mikoa tuliyoifikia ni pamoja na Tanga, Morogoro, Dodoma na Dar es Salaam yenyewe ambayo ndio kituo. Tunaamini utafiti huu utaweza kusanifu majengo yatakayotumia nishati kidogo kwenye hatua ya ujenzi wake na hata wakati wa matumizi ya majengo husika” alieleza Mhandisi Benedict Chilla.

Kwa upande wake, Mhandisi Heri Hatibu amebainisha kuwa,  katika utafiti huo wanatumia mambo mbalimbali ya kitaalamu ambayo yanahitaji uwelewa wa hali ya juu kuyabaini ikiwemo kukokotoa kiasi cha vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi wa nyumba.

Aidha, HHBRA wameeleza kuwa, utafit huo umefanyika kwenye maeneo kadhaa ikiwemo vifaa vya kujengea kuta,(Matofali ya kuchoma, matofali ya mchanga saruji, matofali ya udongo saruji ya kufungamana.

Pia vifaa vya ujenzi wa dari (slab) kwa nyumba yenye ghorofa moja na kuendelea ambapo utafiti wake bado unadelea (dari la  zege na nondo, ‘Laad’s, pamoja na ‘waffle’.

Hata hivyo wataalamu hao wamebaini kuwa matofali ya kuchoma yamekuwa yakichangia hewa ukaa nyingi kutokana na maandalizi yake ambapo pia ni miongoni mwa vifaa vya ujenzi vinavyochangia uharibifu wa mazingira kwa wakati wa maandalizi kwa kutumia kuni nyingi ilikuyachoma

DSC_5233Mkandarasi wa NHBRA,  Muhandisi Benedict Chilla akifafanua jambo katika mkutano huo kwa wanahabari ( Hawapo pichani) mapema leo jijini Dar es Salaam. anayemfuatia ni Kaimu Mkuu wa kitengo cha Habari na Masoko wa NHBRA, Bi. Zubeda Salum

DSC_5243Mkandarasi wa NHBRA, Mhandisi Heri Hatibu akifafanua jambo namna utafiti  huo (Kwa wanahabari hawapo pichani) utakavyoweza kusaidia Taifa katika masuala ya ujenzi na kuzuia gesi ukaa. Anayemfuatia ni Kaimu Mkuu wa kitengo cha Habari na Masoko wa NHBRA, Bi. Zubeda Salum

DSC_5257Kaimu Mkuu wa kitengo cha Habari na Masoko wa NHBRA, Bi. Zubeda Salum akifafanua jambo katika mkutano huo. kulia kwake ni Mkandarasi wa NHBRA,  Muhandisi Benedict Chilla na kushoto ni Mkandarasi wa NHBRA, Mhandisi Heri Hatibu. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

Share:

Leave a reply