Wakimbizi 26,000 kutoka Somalia wazuiliwa kwenda Marekani

752
0
Share:

Ni wazi agizo la Rais mpya wa Marekani, Donald Trump la kuzuia wakimbizi kutoka nchi saba zenye imani kali ya Kiislamu zinaendelea kuwagusa watu wengi kwa jinsi muda unavyokwenda hali inayofanya watu wengi wa ndani na nje ya nchi ya Marekani kumwona Trump kama kiongozi ambaye anakiuka haki za binadamu.

Agizo la Trump lilizuia wakimbizi kutoka Iran, Iraq, Syria, Libya, Somalia, Sudan na Yemen na wataruhusiwa kuingia Marekani baada ya hali ya usalama kuimarishwa kwani kwa sasa kuna hofu ya kutokea matukio ya kiharifu ambayo Trump anahisi wakimbizi hao ndiyo wanaweza kuyafanya kama wakiingia sasa.

Baadhi ya wakimbizi ambao wameathirika ni wakimbizi 26,000 wa Somalia waliopo Kenya ambao jumatatu ya Januari, 30 walitarajiwa kuanza kuondoka Kenya na kupelekwa Marekani lakini baada ya Trump kutoa agizo ijumaa safari hiyo imesimamishwa.

Baadhi ya wakimbizi hao wamesema kuwa agizo ambalo amelitoa Trump limewaumiza kwani ndoto zao zilikuwa zimekaribia kutimia lakini yeye amefanya maamuzi ya kuwazuia wasiende, “Trump amekatisha ndoto zetu.”

Nusu ya wakimbizi hao ambao wapo kwenye kambi ya wakimbizi iliyopo Nairobi walikuwa wameshapatiwa vibali vya kuingia Marekani na nusu yao walikuwa wakisubiri kufanyiwa mahojiano na maafisa kutoka Marekani ili nao wapate vibali vya kuingia Marekani.

Share:

Leave a reply