Walioshindwa kukamilisha agizo la JPM kupewa madawati ya bure

234
0
Share:

Baada ya kumalizika kwa muda uliotolewa na Rais Magufuli wa kila mkoa kuhakikisha inakuwa na madawati ya kutosha kwa shule zote na baadhi ya mikoa kushindwa kukamilisha agizo hilo taasisi ya Dk. Amon Mkoga imejitoa kusaidia baadhi ya mikoa madawati.

Akizungumzia misaada ya madawati ambayo watakuwa wakiitoa, Mkurugenzi wa Taasisi ya Dk. Amon Mkoga, Dk. Amon Mkoga amesema kuwa misaada hiyo itatolewa kwa mikoa ya Tabora na Pwani na itaambatana na kampeni ya SIMAMA KAA DESK CAMPAIGN.

Amesema kuwa mpaka sasa wameshatoa madawati 400 kwa shule za mkoa wa Tabora na wanajipanga kutoa madawati mengine 200 hivi karibuni ili kuhakikisha agizo la rais linakamilika kama ilivyo matarajio yake.

“Taasisi yetu inahusika na kusaidia elimu na kwa kuanza tunatoa misaada kwa mkoa wa Tabora na Pwani, hatua hii ni kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli za kuhakikisha tunaondokana na changamoto ya madawati,

“Tunatambua kuwa kuna changamoto nyingi lakini madawati haya ambayo niya chuma na mbao yatasaidia kwa kiasi fulani na baada ya muda tutajipanga kutoa misaada mingine ambayo inamahitaji makubwa kwa wanafunzi,” alisema Dk. Mkoga.

Share:

Leave a reply