Wambura afungiwa maisha kujihusisha na soka

330
0
Share:

Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) imemfungia maisha kutojihusisha na mchezo wa mpira wa miguu Makamu wa Rais wa shirikisho hilo, Michael Wambura baada ya kukumkuta na hatia ya kutumia cheo chake vibaya kwa kujipatia fedha haramu.

Uamuzi huo umetangazwa mchana wa leo na kamati hiyo baada ya kufanya kikao jana kujadili tuhumza za Wambura ambapo ilimkuta na hatia ya makosa matatu, ikiwemo kupokea fedha za TFF za malipo ambayo hayakuwa halali.

Pamoja na kughushi barua ya kueleza alipwe malipo ya Kampuni ya Jeks System Limited huku akijua kwamba hayakuwa halali.

Hata hivyo Wambura anadaiwa kutaka kuzungumza na wanahabari mchana wa leo, huku Wakili wake Emanuel Muga akidai kuwa Wambura hakupewa nafasi ya kumtetea mteja wake.

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply