Wanafunzi ni 917,072 kufanya mtihani wa darasa la saba

970
0
Share:

Baraza la Taifa la Mitihani nchini (NECTA) limesema maandalizi ya kuanza mtihani wa Taifa wa darasa la saba utakaofanyika siku ya jumatano Septemba 6 na alhamisi ya Septemba 7 yamekamilika.

Akizungumza na wanahabari kuhusu maandalizi hayo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde. Tayari mitihani imesafirishwa katika maeneo yote nchini na kinachosubiriwa kwa sasa ni kuanza kwa mtihani.

“Kesho na kesho kutwa katika shule zetu 16,583 za msingi nchini kutakuwa ana mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, watahiniwa ni 917,072 wataufanya wavulana wakiwa 432,744 sawa na asilimia 47.19%, wasichana ni 484,328 sawa na asilimia 52.81%, mwaka jana watahiniwa walikuwa 795,761,

“Mitihani yote imesafirishwa kwenye halmashauri zote nchini … mitihani hii ni muhimu kujua uelewa wa wanafunzi kwa masomo ya darasa la saba lakini pia kuchagua wanafunzi wa kujiunga na masomo ya sekondari hivyo mitihani hii ni muhimu kwa wanafunzi, wazazi na jamii nzima,” amesema Dk. Msonde.

Katibu Mkuu huyo wa NECTA amesema watahiniwa 88,349 watafanya kwa lugha ya Kiswahili na watahiniwa 34,823 watafanya kwa lugha ya Kiingereza na masomo ambayo yatafanyiwa mtihani ni Kiswahili, Kiingereza, Sayansi, Hisabati na maarifa ya Jamii.

 

Aidha Dk. Msonde amewataka wasimamizi kufuata taratibu zote zinatotakiwa kufuatwa wakati wa kusimamia wanafunzi wawapo kwenye chumba cha mtihani na kwa wanafunzi wahakikishe wanakuwa makini wawapo kwenye chumba vya mtihani ili waweze kujibu maswali kwa ufasaha.

Share:

Leave a reply