Wanamgambo wavamia Chuo cha Polisi Pakistan na kuua wanafunzi, walinzi

259
0
Share:

Wanafunzi wa upolisi na walinzi 58 wa Chuo cha Polisi Balochistan kilichopo Quetta, Pakistan wanaripotiwa kupoteza maisha baada ya kutokea mlipuko chuoni ambao unakisiwa kufanywa na wanamgambo.

Taarifa zinaeleza kuwa walionekana wanamgambo watatu wakiingia eneo la chuo wakiwa wamefunika sura zao huku wakiwa wamevaa mabomu ambayo waliyatumia kufanya mlipuko.

Baada ya shambulizi hilo, polisi wengine waliokuwa eneo hilo walifanikiwa kuwashambulia watu hao na kuwaua na mpaka sasa hakuna kikundi chochote ambacho kimejitangaza kuhusika na shambulizi hilo.

Mamia ya wanafunzi wa chuo hicho wamehamishwa kutoka katika chuo hicho cha upolisi cha Balochistan na polisi wameongezwa eneo la chuo ili kuimarisha ulinzi.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, mmoja wa wanafunzi ambao walilishuhudia alisema, “Niliwaona wanaume watatu wakiwa wamefunika sura zao na wakiwa wameficha silaha aina ya kalashnikovs, walianza kupiga risasi katika mabweni na mimi nilikimbia kwa kuruka ukuta”

Share:

Leave a reply