Wananchi Singida waadhimisha miaka 53 ya Muungano kwa kufanya usafi

430
0
Share:
Wakazi wa Manispaa ya Singida wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Elias Tarimo, wameadhimisha sherehe ya maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutimiza miaka 53 kwa kufanya usafi katika sehemu mbalimbali za mji wa Singida.
 
Akizungumza baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi, Dc Tarimo alisema Watanzania wakiwemo wa wilaya ya Singida, wanapaswa kuuenzi Muungano huu kwa kushiriki kikamilifu maadhimisho yake.
 
Amesema bila Muungano huu ulioasisiwa na viongozi wetu hayati mwalimu Nyerere na mzee Abeid Karume, Tanzania ya leo isingekuwepo.
 
“Maadhimisho haya sasa yameboreshwa kwa maana yanaweza kufanyika kwa kufanya usafi kama tulivyofanya sisi leo,au kwa mazoezi ya mwili.Niwasihi tu Watanzania wenzangu kuyathamini maadhimisho haya na kushiriki bila kukosa kila mwaka,” alisema.
 
Kwa upande wake mkurugenzi manispaa ya Singida, Bravo Lyampembile, alisema wananchi wa manispaa hiyo wamejitokeza kwa  na kushiriki vema kuadhimisha siku kuu ya Mungano.
 
“Ofisi yangu nayo imeshiriki watumishi wote ambao kwa siku ya leo afya zao ziko vizuri, wamejitikeza na kufanya usafi kama njia ya kuadhimisha siku kuu ya Muungano,” alisema Bravo.
Na Nathaniel Limu, Singida
Share:

Leave a reply