Wanawake TBL Group wajiunga na programu ya mwanamke wa wakati ujao ya ATE

207
0
Share:

Wanawake watatu kutoka kampuni ya TBL Group wamechaguliwa kujiunga na mpango wa mwanamke wa wakati ujao ambao imeanzishwa na Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa kushirikiana na Shirikisho la Vyama vya Waajiri nchini Norway ambao umeenga kuboresha ufanisi wa wafanyakazi wa kike mahali pa kazi hapa nchini.

Mpango huu ambao umezinduliwa jijini Dar es Salaam unawashirikisha wanawake wapatao 33 kutoka makampuni mbalimbali nchini ambao watapatiwa mafunzo mbalimbali ya uongozi.

Akiongea kwa niaba ya wenzake Meneja wa kuendeleza vipaji wa TBL Group Lilian Makau Galinoma ambaye amechaguliwa kushiriki katika mpango huu alisema  wanashukuru kampuni yao kwa kuona umuhimu wa kuendeleza wafanyakazi wake.

“Tunaishukuru kampuni yetu kwa kutufadhili ili tuweze kupata mafunzo ya uongozi na tuna imani yatatupa upeo zaidi wa kuboresha utendaji wa kazi zetu za kila siku ikiwemo kuendeleza vipaji vya wafanyakazi wenzetu wa kike  “.Alisema.

Meneja wa kuendeleza Vipaji wa TBL Group Lilian Makau Galinoma

Meneja wa kuendeleza  Vipaji wa TBL Group Lilian Makau Galinoma akitoa mada wakati wa uzinduzi wa mpango wa Mwanamke wa wakati  ujao Tanzania (Female Future Tanzania) ulioanzishwa na Chama Cha waajiri Tanzania( ATE) .Uzinduzi ulifanyika katika iliyofanyika hoteli ya Sea Cliff  jijini Dar es Salaam.

vipaji tbl 13

Baadhi ya washirki wa Warsha ya Mwanamke wa Wakati Ujao Tanzania (FEMALE FUTURE TANZANIA) wakimsikiliza  mada mbalimbali zilizotolewa wakati wa uzinduzi wake  katika  haoteli ya Sea Cliff   jijini Dar es Salaam.

vipaji tbl 14

Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dk.Aggrey Mlimuka

Mkurugenzi Mkuu  wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dk.Aggrey Mlimuka (kulia) akimpongeza  Meneja wa kuendeleza  Vipaji wa TBL Group  Lilian Makau Galinoma mara baada ya kumaliza kutoa mada wakati wa uzinduzi wa Progamu ya Mwanamke wa wakati ujao Tanzania (Female Future Tanzania) iliyoandaliwa na Chama cha waajiri Tanzania ( ATE) katika hoteli ya Sea Cliff  jijini Dar es Salaam.

vipaji tbl 7

Mkurugenzi Mkuu  wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Dk.Aggrey Mlimuka (wa pili kulia) akibadilishana mawazo na  Meneja  Vipaji wa TBL Group  Lilian Makau Galinoma (wa pili kushoto) wakati wa uzinduzi wa mpango wa Mwanamke wa wakati ujao Tanzania (Female Future Tanzania) utakaoendeshwa  na Chama cha waajiri Tanzania (ATE). Kushoto ni Meneja bidhaa wa Kiwanda cha  Konyagi (DTL) Warda Kimaro na Meneja Mkuu mpishi wa pombe wa Chibuku. (DARBREW) Neema Arora. Uzinduzi umefanyika katika hoteli ya Sea Cliff jijini Dar es Salaam.

vipaji tbl 6

Watendaji waandamizi wa taasisi mbalimbali wakiwa katika picha ya washiriki wa mpango wa   Mwanamke wa wakati  ujao Tanzania (Female Future Tanzania) wakati wa uzinduzi wake katika hoteli ya  Sea Cliff jijini Dar es Salaam.

Share:

Leave a reply