Wapalestina waitangaza Ijumaa kuwa “Siku ya Hasira”

315
0
Share:

Vikundi vya Wapalestina mjini Yerusalemu vimeiita siku ya Ijumaa kuwa ni “Siku ya Hasira” baada ya kufanya maandamano jana Alhamisi ya kupinga tangazo la Rais wa Marekani Donald Trump, la kuutambua mji huo kama mji mkuu wa Israeli ambapo watu takribani 31 waliripotiwa kujeruhiwa na risasi za kijeshi.

Licha ya hatua hiyo, Kikundi cha Kiislamu cha Hamas kimewataka Wapalestina kuachana na juhudi za amani na kuzindua “Intifada” mpya dhidi ya Israeli kufuatia Trump kutangaza kutambua Yerusalemu kama mji mkuu wake.

Siku ya Ijumaa ambayo imepewa jina la “Hasira” kunatarajiwa kufanyika maandamano kwenye vituo vya ukaguzi vinavyolindwa na Israeli na kando ya mpaka wa Gaza.

Kufuatia mgogoro huo, Wapalestina wameripotiwa kutotaka mazungumzo na Marekani ili kutafuta suluhu, ambapo Afisa Mkuu wa Palestina na fatah alisema Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence anaetarajiwa kufanya mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Mahmoud Abbas, hatokaribishwa nchini humo.

Share:

Leave a reply