Wapiganaji wa ADF wadaiwa kuhusika na mauaji ya askari wa Tanzania

211
0
Share:

Ripoti Maalumu ya Uchunguzi uliofanywa na Umoja wa Mataifa imekitaja kikundi cha waasi wa Alliance Democratic Forces (ADF) kwamba kilihusika na mauaji ya askari wa Tanzania yaliuyotokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Ripoti hiyo imebainisha kuwa, ushahidi uliopatikana unaonyesha ADF ndiyo mhusika wa shambulizi hilo lililotokea Januari 5 mwaka huu, ambapo walifaya shambulizi la kushtukiza lililosababisha vifo vya walinda amani hao.

Vilevile timu hiyo maalumu ilipewa jukumu la kuchunguza tukio la shambulizi la Desemba 7, mwaka jana ambapo walinda usalama 15 wa Tanzania waliuawa katika kituo chao Semuliki, huku 43 wakijeruhiwa na mmoja mpaka sasa hajulikani alipo.

Uchunguzi huo pia umehusisha mashambulizi mawili ya awali dhidi ya walinda usalama wa Tanzania yaliyotokea karibu na Mamundioma Septemba 16 na Oktoba 7, 2017.

Share:

Leave a reply