Wapiganaji wa Al Shabab wavamia nyumba ya kulala wageni na kuua watu 12

290
0
Share:

Watu 12 wanaripotiwa kupoteza maisha wakiwa katika nyumba ya kulala wageni (Bishaaro Hotel lodge) katika mji wa Mandera, Kenya baada ya wapiganaji wa kikundi cha Al Shabab kuvamia katika nyumba hiyo na kufanya shambulizi usiku wa kuamkia leo.

Kamanda wa Polisi wa Mandera Mashariki, Ezekiel Singoe amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kuwa watu 10 kati ya waliouliwa ni wanafunzi ambao walikuwa wamefanya vizuri katika masomo yao ya sekondari na walikuwa katika mji huo kwa ajili ya kukabidhiwa vyeti vyao.

Singoe amesema kwa sasa bado miili ya marejemu haijafahamika na ndugu zao na taratibu zinaendelea.

Amesema watu hao walipofika katika nyumba hoteli hiyo walitumia mlipuko kuvunja mlango kisha kuingia ndani ambao waliingia katika vyumba ambavyo walikuta watu na kuwaua.

Share:

Leave a reply