Wapiganaji wawili wa kundi la IS wakamatwa

77
0
Share:

Raia wawili wa nchini Uingereza wanaodhaniwa kuwa wanachama wa kikundi cha wapiganaji wa Dola ya Kiislam (IS) wanashikiliwa na kundi la wapiganaji wa Kikurd.

Watu hao ambao walikuwa wanasakwa kati ya wenzao waliokwisha kamatwa, ni Alexanda Kotey mwenye umri wa miaka 34 na El Shafee Elsheikh mwenye miaka 29.

Taarifa zinaeleza kuwa, raia hao wa Uingereza ndani ya kundi la IS walikuwa na kundi hatari linalofahamika kama Beatles waliotambulika kutokana na lafudhi yao wanapozungumza. 

Maafisa wa Marekani wamesema kundi hilo lililokuwa likihusika na utoaji mateso pamoja na kuua ndani ya IS, linadaiwa kuwachinja zaidi ya watu 27 mateka kutoka nchi za kimagharibi na kutoa mateso makali kwa wengine wengi tu.

Share:

Leave a reply