Wapinzani, kabila jino kwa jino, wamtaka ajiuzulu

375
0
Share:

Kiongozi wa upinzani na tajiri Moise Katumbi amesema lazima Rais wa Congo, Joseph Kabila aheshimu katiba na kuachia madaraka kwa Amani kwa kuruhusu uchaguzi huru na wa haki ufanyike mara mmoja .

Katumbi, mwanasiasa maarufu zaidi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa mujibu wa duru za kisiasa nchini huo, ameitaka jumuiya ya kimataifa kuingilia kati mgogoro wa Congo ili kunusuru nchi hiyo kuingia kwenye machafuko na umwagaji wa damu wa raia wasio kuwa na hatia.

DRC ni nchi yenye kila aina ya utajiri lakini hivi karibuni imekuwa na maandamano ya vurugu ya kumtaka rais Kabila, aachie ngazi kwa amani bila umwagaji wa damu.

Duru za siasa na vyombo vya habari vinasema kwamba mamia ya polisi wenye silaha wamewekwa kwenye vituo vya ukaguzi karibu na mji wa Kinshasa, huku askari wakiwa katika magari ya kivita.

moise-katumbi

Moise Katumbi

Wachunguzi wa mambo wanahofia watu maskini zaidi wanaweza kuwa katika hali mbaya endapo hali hii ya sintofahamu ikiendelea.

Katumbi, gavana wa zamani wa mkoa wa kusini wa Katanga, ni mmoja wa wagombea wanaotishia nafasi ya rais kabila katika uchaguzi uliotazamiwa kufanyika mwaka huu mapema ambao umeahirishwa mpaka 2018.

Kwa mujibu wa katiba ya Congo, Rais Kabila alipaswa kuachia madaraka leo tarehe 19 lakini kwakuwa uchaguzi haukufanyika kama ulivyopagwa.

Share:

Leave a reply