Warusi wapiga kura kubadili jina la mtaa kuwa Donald Trump

511
0
Share:

Wakazi wa mji wa Ryazan nchini Urusi wameonyesha mapenzi yao waziwazi kwa Rais mteule wa Marekani, Donald Trump kwa kutaka kubadili jina la mtaa mmoja mjini humo kutoka jina la Godbless na kuwa Donald Trump.

Jambo hilo linaonekana kuwashangaza watu wengi kwani Urusi na Marekani kwa muda mrefu zimekuwa zikipishana kauli katika mambo mbalimbali kwa uongozi wa Rais wa Urusi, Vladimir Putin na Rais wa Marekani, Barack Obama lakini kwa Trump mambo yanaonekana kuwa tofauti kwani mpaka sasa zaidi ya watu 300 wamesaini pendekezo wakitaka mtaa ubadilishwe jina.

Mkazi mmoja wa eneo hilo, Sergey Bizyukin amesema awali mtaa huo ulipewa jina la Godbless katika kipindi cha Ukomunisti wakati ambao wakazi wa eneo hilo walikuwa hawaamini dini lakini kwa sasa wananchi wamedhamiria kubadili jina.

“Wengine wanaona ni utani na kusaini sababu ni jambo la kufurahisha, wengine wanaelewa ni sehemu ya kusuluhisha uhusiano wa Marekani na Urusi, na wengine wanasaini sababu hawalipendi jina la mtaa la Godbless,” alisema Bizykin.

Share:

Leave a reply