Wasanii 400 kushiriki tamasha la Sauti za Busara 2018

391
0
Share:

Zaidi ya Wasanii 400 wanatarajia kuonesha uwezo wao kwenye tamasha la Sauti za Busara 2018, linalotarajia kufanyika Februari 8-11, katika viunga vya Ngome Kongwe, Unguja, Zanzibar.

Wasanii hao 400 kutoka mataifa mbalimbali Duniani wanatarajia kuonesha shoo 44 kwa muda huo wa siku nne katika majukwaa matatu tofauti likiwemo la Ngome Kongwe (Old Fort) na jukwaa la wazi la Bustani ya Forodhani (Forodhani Gardens), kuanzia siku hiyo ya  Februari 8 – 11,2018.

Wasanii hao wote wanatarajia kupiga muziki wao kwa kutumia vifaa moja kwa moja ilikupata radha halisi ya muziki ambao utakuwa ni wa ‘live’.

Wasanii hao na bendi pamoja na nchi wanazotoka ni pamoja na: Kasai Allstars (DRC), Zakes Bantwini (South Africa)  Alsarah & the Nubatones (Sudan / USA)  Msafiri Zawose (Tanzania).

Wasanii wengine ni  Ribab Fusion (Morocco)  Kidum & the Boda Boda Band (Burundi / Kenya)  Mlimani Park Orchestra (Tanzania), Afrikan Boy (Nigeria / UK)  Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta (Zanzibar)  Matona’s Cultural Band (Zanzibar / Tanzania).

Pia wapo Makadem (Kenya)  Mangwenya Diana Samkange (Zimbabwe),  Fatma Zidan (Egypt / Denmark)  Inganzo Ngari (Rwanda)  Mzungu Kichaa (Tanzania / Denmark)  Segere Original (Tanzania)  Simangavole (Reunion)  Jally Kebba Susso (Gambia)  Maia & the Big Sky (Kenya).

Wengine ni  Kiltir (Reunion)  El Dey (Algeria)  Maulidi ya Homu ya Mtendeni (Zanzibar)  Simbin Project (Switzerland)  CAC Fusion (Tanzania)  Mbanaye (Malawi)  Ernest Ikwanga (Malawi)  Isack Abeneko (Tanzania).

Pia wapo msanii  Grace Matata (Tanzania)  Safi Theatre (Tanzania)  Siti & the Band (Zanzibar)  Matona’s Afdhal Group (Zanzibar / Norway)  Mapanya Band (Zanzibar / Norway)  na  Zanzibar Taarab Ensemble (Zanzibar). Hao ni baadhi ya wasanii watakaokuwapo kwenye Sauti za Busara 2018.

Aidha, tamasha hilo limekuwa miongoni mwa matamasha makubwa Barani Afrika huku pia likielezwa kuwa moja ya matamasha yanayochangia fursa za kiuchumi visiwani Zanzibar ikiwemo kukuwa kwa biashara ya Utalii.

 

 

Share:

Leave a reply