Washindi wa shindano la European Youth Film Competition (EYFC) 2017 wapatikana

540
0
Share:

Washindi wa Shindano la European Youth Film Competition 2017, usiku wa jana wa Septemba 16, wameweza kupatikana baada ya filamu zao kuibuka kidedea katika shindano hilo lililozinduliwa rasmi  Mei 29, 2017,  ambapo ni kwa mara ya kwanza  kufanyika nchini.

Tukio hilo la kuwapata washindi limefanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta Jijini Dar es Salaam na kuudhuliwa na wadau mbalimbali wa tasnia ya filamu hapa nchini ambapo pia walishudia baadhi ya filamu zilizoingia tano bora na kupata mshindi.

Miongoni mwa washindi hao walioingia tano bora kutokana na kutengeneza filamu fupi ni pamoja na Dennis Chacha, Freddy Feruzi, Louis Shoo, Rashid Songoro na Taragwa Anthony.

Awali wakati wa kutangazwa kwa washindi hao, Balozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya (EU) Nchini, Balozi Roeland Van de Geer aliwapongeza washiriki wote walioonyesha uthubu wao wa kuandaa na kutuma kazi zao kwa kushindaniwa licha ya kuwapata washindi lakini aliwataka wasikate tamaa.

 ‘Filamu hizi tano bora zilizochaguliwa zilikuwa na maandalizi mazuri na hakika  kwani zimeweza kukidhi kauli mbiu ya shindano husika, zipo na ubora unatakiwa na zimekidhi vigezo hivyo hongereni sana  alieleza Balozi Roeland Van de Geer.

Baadhi ya Majaji (mstari wa mbele) pamoja na wageni wengine waalikwa wakifuatilia kilele cha fainali za shindano hilo jana usiku katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa.

Katika filamu hizo tano bora ziliweza kuchaguliwa na jopo la majaji wabobezi  akiwemo Richard Ndunguru, Issa Mbura, Amil Shvji, Deepesh  Shapriya. Wengine Majaji waalikwa akiwemo Tulanana Buhohela, Dk. Vincensia Shule  na Kantarama Gahigiri.

Filamu hizo fupi tano bora zilizoshinda ni pamoja na’Shida za Uani’ iliyotengenezwa na Taragwa Anthony  ambaye alishinda mshindi wa kwanza na kujinyakulia Tshs 7 millioni, mshindi mwingine  ni Rashid Songoro kupitia filamu yake ya ‘Tone’ alishinda Tshs 5million na nyingine ni filamu ya Makala ‘documentary’ mshindi ni Fred Feruzi aliondoka na kitita cha Tshs 3 millioni.

Mshindi mwingine ni Luis Show, kupitia filamu yake fuopi ya ‘Watoto Wangu’ na mshindi mwingine ni Wambura Mwikabe kupitia filamu yake iliyokuwa mtindi wa Makala, ‘Watu na Samaki’ ambayo ilishinda tuzo za chaguo la watu.

 Balozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya (EU) Nchini, Balozi Roeland Van de Geer akimkabidhi hundi ya mfano mshindi wa Milioni 7, kupitia filamu yake ya ‘Shida za Uani’, Bw. Taragwa Anthony  ambaye alishinda mshindi wa kwanza na kujinyakulia  fedha hizo.

Mashindano hayo yaliandaliwa kwa pamoja na Umoja wa Ulaya (EU) na washirika nchi za Netherlands, United Kingdom, Ubalozi wa Ufaransa, Alliance Française, British Councils pamoja na Bodi ya Filamu nchini Tanzania.

Katika shindano hilo vijana mbalimbali nchini,  walipata fursa ya kuzungumzia mijadala ya maendeleo likiwemo suala la Ongezeko la idadi ya watu nchini Tanzania, Afrika na Duniani. Huku filamu shindaniwa wakitakiwa kuziandaa kutoka katika  Swali  la “Ikiwa Je suala hilo ni changamoto au fursa ya maendeleo? Ambapo walitakiwa kuandaa filamu yenye muda wa kuanzia sekunde, ama dakika moja hadi 5 au 10, huku zikiwa katika aina yoyote, iwe ‘Documentary’, Maigizo lakini iwe dakika 5 au 10 katika Maudhui hayo huku washiriki walikuwa vijana wenye umri kati ya miaka 18-35.

Mmoja wa Majaji wa shindano hilo akizungumza wakati wa fainali hizo jana Septemba 16,2017, Jijini Dar es Salaam.

 Bw. Taragwa Anthony akiwa na hundi yake ya  mfano mshindi wa Milioni 7, kupitia filamu yake ya ‘Shida za Uani’, alishinda mshindi wa kwanza na kujinyakulia  fedha hizo.

 Balozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya (EU) Nchini, Balozi Roeland Van de Geer akimkabidhi zawadi kwa washindi  wa shindano hilo.

 Balozi wa Nchi za Umoja wa Ulaya (EU) Nchini, Balozi Roeland Van de Geer akimkabidhi zawadi kwa washindi  wa shindano hilo.

Share:

Leave a reply