Wasomi Marekani wapinga pendekezo la Trump kuongeza kodi kwa bidhaa za Mexico

777
0
Share:

Baada ya kufanikiwa kupitisha mpango wake wa tangu akigombea Urais wa kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico kwa kigezo cha kuzuia wahamiaji, Rais wa Marekani, Donald Trump amekuja na mpango mpya ili kufanikisha ujenzi huo.

Trump kupitia msemaji wake, Sean Spicer amependekeza kuwa bidhaa zote za Mexico ambazo zitakuwa zikiingia Marekani zitozwe kodi ya asilimia 20 ili pesa ambayo itapatikana itumike kugharamia kujenga ukuta.

Spicer alisema kama bidhaa hizo zitatozwa kwa kodi ya asilimia 20 pesa za kujenga ukuta zitapatikana kwani nia ya Trump ni pesa zote ambazo zitatumika kujenga ukuta zitoke Mexico na sio Marekani kwani hakuna pesa iliyotengwa kwa ajili ya ujenzi huo.

Akitoa maoni kuhusu mpango huo, Mwanauchumi kutoka Chuo Kikuu cha Texas Tom Fullerton amepinga kwa kuwa mpango huo utaathiri uchumi wa Marekani kwani kuongeza kodi ni kuathiri viwanda vya nchi hiyo ambavyo baadhi yake hutumia malighafi kutoka Mexico.

“Utaadhiri utendaji kazi wa viwanda badala ya kusaidia, utasababisha kupunguza ajira  kuliko ulivyo sasa,” alisema Fullerton.

Nae Rais wa Wafanyabiashara wa Texas (TAB), Chris Wallace amepinga mpango huo akitolea mfano mji kama Texas  kuwa uchumi wake uwepo unahitaji sana kushirikiana na Mexico ambayo wanapanaka nayo,

“Mshirika mkubwa wa biashara za Texas ni Mexico, kuweka tozo ya kodi kufikia asilimia 20 kutaathiri uchumi wa Texas, mpango huo unamaana ya kutokuwepo ajira na kushusha uchumi wa taifa,” alisema Wallace.

Share:

Leave a reply