Wataalamu wa afya nchini kutafuta mbinu ya kuongeza muda wa mtu kuishi

568
0
Share:

Wataalamu wa masuala ya afya nchini wanatarajiwa kukutana kwa ajili ya kubadilishana pamoja na kutafuta mbinu za kinga na tiba ya magonjwa mbalimbali ili kuboresha afya za watanzania sambamba na kuinua kiwango cha kuishi. 

Hayo yameelewa leo Mei 19, 2017 jijini Dar es Salaam, na Mjumbe wa Chama cha Afya ya Jamii nchini (THPA) Dkt. Mashombo Mkamba wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“TPHA inatarajia kufanya mkutano wake wa 34 hivi karibuni, ambao umelenga kukutanisha wataalamu mbalimbali wa afya kwa ajili ya kubadilishana mbinu za kinga na tiba kwa magonjwa,” amesema na kuongeza.

“Wataalamu hao wataunganisha nguvu zao ili kuweza kupambana na magonjwa hatarishi na kuboresha afya za watanzania sambamba na kuinua kiwango cha kuishi ili watu waishi muda mrefu. Kwa sasa ukomo wa kuishi kwa watanzania ni miaka 60, wakati watu wa Japani ukomo wao ni miaka 80 kuendelea.” amesema Dk. Mkamba.

Aidha, Dkt. Mkamba amewataka watanzania kujenga desturi ya kuchangia damu mara kwa mara, kwa kuwa kitendo hicho kinasaidia kujua afya zao pindi wanapopimwa kabla ya kufanya zoezi la utolewaji damu, pia kitasaidia kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji damu.

“Watanzania wengi bado hawajui umuhimu na faida ya kujitolea damu, mfano mtu anaporuhusiwa kutoa damu anakuwa amepimwa vipimo vyote na kwamba ikibainika kuwa hana magonjwa yuko safi kiafya huruhusiwa kufanya hivyo. Kwa hiyo kwa sisi wataalamu tunaona hiyo ni faida kwani unapimwa na kujua afya afya. Hali kadhalika unapochangia damu, unaruhusu damu mpya kuzalishwa,” amesema.

 Na Regina Mkonde  

Share:

Leave a reply