Watanzania waaswa kufanya mazozi kuepuka ugonjwa wa kisukari

512
0
Share:

Watanzania waaswa kujihusisha na tabia ya kupenda kufanya mazoezi ili kuepuka ugonjwa wa kisukari na viashiria vyake katika jamii yetu inayotuzunguka.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Kinga Wizara ya afya Dkt. Neema Rusibamayila alipomwakilsha Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa kuadhimisha siku ya Kisukari duniani leo jijini Dar es salaam.

“Watanzania tunatakiwa kupenda kujijengea tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuweza kuepuka magonjwa yasioambukiza ikiwemo Kisukari na viashiria vyake kwa ujumla,” alisema Dkt. Rusibamayila.

Aidha Dkt. Rusibamayila amesema kuwa watanzania wengi hawana budi kujikinga na ugonjwa huo kwani asilimia 60 wanafariki kwa ugonjwa huo duniani kila mwaka.

Kwa mujibu Wa Dkt. Rusibamayila amesema kuwa asilimia kubwa ya wanawake nchini wana uzito mkubwa,mafuta mengi na hawajihusishi na mazoezi hivyo hupelekea kupata hathari za ugonjwa wa kisukari.

Mbali na hayo Dkt. Rusibamayila amesema kuwa licha tu ya kufanya mazoezi lakini pia wanatakiwa kuepuka matumizi ya vileo kama vile uvutaji tumbaku,unywaji pombe na uvutaji wa shisha ili kuepuka magonjwa yasioambukiza kwani yamekuwa hatari kwa watanzania.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha chakula na Lishe (TFNC) Dkt. Vicent Assey amesema kuwa sambamba na kufanya mazoezi watanzania wanatakiwa kuzingatia mlo ulio bora ili kuepuka ugonjwa wa kisukari.

Aidha Dkt Assey amesisitiza walimu , wazazi na watoa huduma ngazi ya jamaii wanatakiwa kuwa kipaumbele katika kuelimisha watoto na jamii nzima kwa ujumla juu ya lishe bora ambayo huleta kinga zidi ya kisukari.

Siku ya kisukari Duniani huadhimshwa Novemba 14 kila mwaka na mwaka huu imeadhimishwa sambamba na matembezi ya hiari na mazoezi ya pamoja kutoka viwanja vya muhimbili mpka Mnazi mmoja na kubeba Kauli mbiu isemayo “MWANAMKE NA KISUKARI “ ikimaanisha wanawake wawe mstari wa mbele katika kupambana na ugonjwa huo.

Na WAMJW, Dar Es Salaam

Share:

Leave a reply