Watanzania watakiwa kutumia fursa za kibiashara Congo DRC

282
0
Share:

Wafanyabiashara na wakulima nchini wametakiwa kutafuta fursa za kibiashara pamoja na kuuza mazao na bidhaa zao nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchi hizi mbili.

Wito huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Afisa Biashara Mwandamizi wa Taasisi ya Kiserikali inayohusika na masuala ya biashara na viwanda TanTrade, Getrude Ngwesheni wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano la kibiashara kati ya Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo linalotarajiwa kufanyika Septemba 22, jijini Lubumbashi linalotarajiwa kukutanisha wafanyabiashara wakubwa 100 kutoka nchi zote mbili.

dsc_0852Afisa Biashara Mwandamizi wa Taasisi ya Kiserikali inayohusika na masuala ya biashara na viwanda TanTrade, Getrude Ngwesheni akizungumza kuhusu kongamano la Tanzania DR Congo Trade Forum.

“Lengo la kongamano hili ni kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya Tanzania na Kongo, pamoja na kuwakutanisha waendeshaji wakubwa wa sekta binafsi nchi hizi mbili . Zaidi ya kampuni 25 kutoka Tanzania zitashiriki kwenye kongamano hilo kujadili ongezeko la biashara, fursa za uwekezaji na ushirikiano kati ya nchi hizi,” amesema.

Ameongeza kuwa ” Kongamano hilo litajadili kuhusu uwekezaji katika kilimo cha biashara ili kuweka mazingira mazuri ya wajasiliamali kuvutiwa kufanya uwekezaji katika sekta hiyo. Nchi ya Kongo inaitegemea Tanzania kupata bidhaa zao hivyo wafanyabiashara na wakulima waitumie fursa hii kutafuta masoko ya bidhaa na mazao yao.”

Ngwesheni amesema kuwa fursa nyingine za kibiashara zilizopo nchini Kongo ni pamoja na biashara ya nishati na madini kutokana kwamba nchi hiyo imeonyesha nia kwenye utafutaji wa nishati na madini katika sekta ya mafuta na gesi hapa nchini.

“Kulikuwa na mashauriano kati ya Wizara ya Haidrokaboni ya Kongo na wizara husika ya Tanzania yaliyofanyika mwezi Agosti yalikuwa na mapendekezo ya kuwezesha jiji la Kinshasa kuuza mafuta yake kupitia mfumo wa bomba la mafuta linapotoka bandari ya Tanga hadi Hoima nchini Uganda, ni wakati wa kampuni kubwa na kati kujitokeza katika kongamano hilo ili kupata fursa hizo ,” amesema.

dsc_0814Mwakilishi wa Waratibu wa Kongamano hilo, Anna Monsa akilezea faida za kongamano hilo.

Mwakilishi wa Waratibu wa Kongamano hilo, TCCIA, Anna Monsa amesema kongamano hilo litakusanya zaidi ya wafanyabiashara 100 ambao watajadili namna ya kuboresha mauzo kati ya nchi zote mbili.

Kongamano hilo limedhaminowa na Chama cha Wafanyabiashara, viwanda na kilimo Tanzania (TCCIA), Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF),  na Shirikisho la Makampuni ya Wfanyabiashara Kongo (FEC).

dsc_0787

Afisa Miradi wa 361 Degrees, Naomi Godwin akielezea dhumini la kongamano hilo.

dsc_0822Kaimu Mkurugenzi wa TPSF, Louis Aecaro akizungumza faida za wafanyabiashara kushiriki kongamano la Tranzania DR Congo Trade Forum.

dsc_0828

Meneja Masoko wa GSM Group of Companies, Farida Rubanza akieleza jinsi kongamano hilo lilivyo na umuhimu kiasi cha kuwashawishi kulidhamini.

Share:

Leave a reply