Watanzania watano wapata nafasi ya kufanya kazi na UN, yupo pia Doris Mollel

743
0
Share:

Tanzania imepata nafasi ya kipekee katika Umoja wa Mataifa (UN) baada ya Watanzania watano kutajwa katika orodha ya vijana 170 ambao wamechaguliwa kuwa mabalozi wa kusaidia kuwainua wanawake kiuchumi duniani.

Watanzania hao ni Agnes Mgongo, Doris Mollel, Hassani Tozir, Catherine Ruge pamoja na Sadick Lungendo. 

Inaelezwa kuwa zaidi ya watu 4,000 kutoka maeneo mbalimbali duniani walituma maombi ili kupata nafasi ya kuwa mabalozi lakini ni watu 170 pekee ambao wamepata nafasi ya kufanya kazi na UN kwa kuwa mabalozi katika mataifa mbalimbali.

Shindano la kutafuta mabalozi 170 wa kuwainua wanawake kiuchumi lilianzishwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia maswala ya wanawake (UN-WOMEN) likiwa na lengo la kuwapata vijana watakaoweza kushirikiana na serikali za nchi zao kuwainua wanawake kiuchumi. 

Utendaji kazi wa mabalozi hao utakuwa ni kushirikiana na Serikali kwa kutoa hamasa kwa wanawake kupitia midahalo mbalimbali ambayo itakuwa ikiandaliwa ili kuwapa elimu jinsi gani wanaweza kujikwamua na janga la umaskini.

Share:

Leave a reply