“Watoto milioni 1.4 Somalia wana utapiamlo mkali”- UNICEF

546
0
Share:

Shirika la Watoto Duniani (UNICEF) limesema Somalia kuna watoto wasiopungua milioni 1.4 ambao wana utapiamlo mkali ikiwa ni ongezeko la asilimia 50 kulinganisha na mwaka uliopita.

Akizungumza kuhusu hali hiyo, Mwakilishi wa UNICEF nchini Somalia, Steven Lauwerier amesema hali ilivyo kwa sasa nchini humo ni mbaya hivyo kunahitajika msaada wa haraka ili kuokoa masiha ya watoto hao.

“Tunatakiwa kufanya jambo la haraka ili kuoa maisha yao, kama misaada haitazifikia familia zilizoathirika, watu wengi watakimbia makazi yao,” alisema Mwakilishi wa UNICEF nchini Somalia, Lauwerier.

Wananchi wa Somalia wamekuwa na kipindi kigumu kutokana na hali ya maisha nchini humo kuwa ngumu kutokana na kukabiliwa na ukame wa muda mrefu sasa hali iliyosababisha wananchi wanaokadiriwa kufikia 615,000 kukimbia makazi yao.

Share:

Leave a reply