“Watu milioni 65.6 duniani hawana makazi ya kuishi”- UNHCR

467
0
Share:

Shirika la Umoja wa Mataifa la Wakimbizi (UNHCR) limesema watu milioni 65.6 wakiwepo wakimbizi na watu wanaotafuta hifadhi duniani kote hawana makazi ya kuishi.

Katika ripoti ambayo imetolewa na UNHCR imesema ripoti hiyo inahusishwa takwimu za hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2016 ambapo kuna ongezeko la watu 300,000 kulinganisha na takwimu za 2015.

Akizungumzia ripoti hiyo, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia wakimbizi, Filippo Grandi alisema takwimu hizo ni kubwa sana kwani inaonyesha jinsi banadamu wengine walivyo kwenye hatari.

“Dunia inaonekana itakuwa sehemu isiyokuwa na utulivu, unaona mtafaruko uliokuwepo awali unazidi kuongezeka na mingine mipya inaibuka na yote inasababisha kusiwepo sehemu nzuri kwa ajili ya makazi,” alisema Grandi.

Share:

Leave a reply