Watu milioni 663 duniani kote wakosa maji safi na salama

600
0
Share:

Katika kuadhimisha siku ya maji duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Machi, 22 ya kila mwaka, Shirika la WaterAid limetoa ripoti ya hali ya upatikanaji wa maji ilivyo kwa sasa duniani.

Katika ripoti hiyo ya WaterAid imeonyesha kuwa kuna watu zaidi ya milioni 660 duniani kote wanakosa maji safi na salama na wengi wao wakiwa ni watu ambao wanaishi maeneo ya vijijini.

“Kwa sasa kuna watu milioni 663 duniani kote ambao wanakosa maji safi na wengi wao wanaofikia milioni 552 wanaishi maeneo ya vijijini,” imesema ripoti ya WaterAid.

Aidha imezitaja nchi ambazo zina hali mbaya zaidi kuwa ni Papua New Guinea, Mozambique and Madagascar na Angola ambayo inangoza ikiwa na asilimia 71 ya wananchi wake wa vijijini wakikosa maji safi na salama.

Pia ripoti ya WaterAid imesema kuwa asilimia 20 ya mataifa yote duniani yameshapata athari kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Share:

Leave a reply