Watu wawili wapigwa risasi na kupoteza maisha katika klabu ya usiku Marekani

228
0
Share:

Matukio ya matumizi mabaya ya silaha yanaendelea kujitokeza nchini Marekani baada ya kuripotiwa taarifa ya watu wawili kupigwa risasi na kupoteza maisha na wengine 16 kujeruhiwa.

Maafisa wa Polisi wamesema kuwa tukio hilo limetokea katika eneo la Fort Myers, Florida katika klabu ya Club Blu majira ya saa sita na nusu usiku.

Aidha Polisi tayari wameanza kufanya uchunguzi wa tukio hilo huku ukiwa na maeneo mawili ambayo yanakisiwa wahusika wa tukio hilo walijihifadhi katika eneo hilo.

Share:

Leave a reply