Wawili wapoteza maisha Geita kwa kukosa hewa

209
0
Share:

Watu wawili wamefariki dunia katika kijiji cha Kanyara kata Kanyara mkoani Geita baada ya kukosa hewa wakati wakichimba kisima kirefu cha Maji.

Wakiongea na MO Blog mashuhuda waliokuwa eneo la tukio wamewataja waliofariki dunia kuwa  ni   Mashauri Kadogo mwenye umri wa miaka 32 na Kulwa Kazimili mwenye umri wa miaka 38 wote wakazi  kijiji hicho cha Kanyara.

 Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mwenyekiti wa kijiji cha Kanyara ambae pia ni baba mdogo wa marehremu, Benjamini Jeremia amesema kuwa wakiwa wanachimba kisima hicho wamekutana na mwamba ambapo waliamua kuwasha moto kwa kutumia mkaa ili kurahisisha kazi wakati wa kuondoa mwamba huo ndipo mwamba huo ulipowaanguakia na kupoteza maisha.

Marehemu hao wamefanikiwa kutolewa katika kisima hicho na taratibu za maziko zinaendelea kufanyika.

Aidha Jeshi la Polisi mkoani Geita limethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Na Emmanuel Twimanye, Geita.

Share:

Leave a reply