Wazee Tabora waomba fedha za TASAF zisitolewe kwa njia ya mtandao

774
0
Share:

Baadhi ya Wazee ambao ni walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini katika Wilaya ya Urambo, Tabora wameuomba Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kuendelea na utaratibu wa zamani wa kuwapelekea fedha mkononi badala ya kutumia kwa njia ya mtandao.

Wazee hao walitoa kauli hiyo katika vijiji mbalimbali vya wilaya ya Urambo ambao walengwa wananufaika na Mpango huo baada ya kukutana timu ya mkoa iliyokwenda kuangalia matatizo wanayokumbana nao katika utaratibu mpya wa ulipaji kwa njia ya mtandao. 

Mmoja wa Wakazi wa Sipungu Mwajuma Shabani alisema kuwa wengi wao hawana simu na hajui kutima simu na hivyo kuwafanya wakati mwingine watafute vijana wa kuwasaidia ambapo baadhi yao uwaibia fedha zao. 

Aliongeza kuwa wengine kwa sababu ya kutojua kusoma na kuandika wakati mwingine wakuwa wakishindwa kutunza kumbukumbu ya namba zao siri na hivyo kuwafanya washindwe kupata fedha pindi inapoingia katika line zao. 

Naye Moshi Rashidi alisema kuwa kikwazo kingine ambacho wanakabiliana nacho ni kuibiwa fedha na watu wanaowaomba msaada wa kuwatolea fedha zilizopo katika line zao zilizotumwa na TASAF. 

Alisema kuwa wakati mwingine wanaomba msaada wa simu ili waweke line zao kwa watoto wao au majirani kwa ajili ya kusaidiwa kutolewa fedha wamekatwa fedha zao na kupata pesa pungufu. 

“Kwa sababu mimi nakuwa sina simu zaidi ya kumiliki line tu wakati mwingine kwa sababu wengi tunawatumia vijana wetu au majirani wenzetu wamekuwa wakiletewa fedha pungufu na wewe uwezi kubisha,” alisema Rashid. 

Aidha Rashid aliongeza kuwa maeneo mengi ya wanufaika wa mpango huo hayana huduma za mawakala wa utoaji wa fedha kwa njia ya mtandoo jambo linalowafanya kusafiri umbali mrefu kutafuta huduma hiyo na wakati mwingine kutumia sehemu ya fedha hizo kulipia nauli ya kwenda na kurudi na hivyo kujikuta wanabaki fedha kidogo sana. 

Awali akitoa elimu kwa Walengwa katika Vijiji vya Kitete na Sipungu juu ya umuhimu wa matumizi ya mtandoo katika upokeaji wa malipo yao, mchumi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fredrick Aron alisema kuwa hivi sasa malipo yote ya Serikali yatolewa kwa njia ya mtandao kwa hiyo ni vema wakaendelea kujifunza jinsi ya matumia ya huduma za utoaji wa fedha kwa njia hiyo. 

Aliongeza kuwa utaratibu na mazungumzo yanaendelea kuhakikisha kuwa mawakala wa kampuni zote za simu watoa huduma ya pesa kwa njia ya mtandao wanahakikisha wanasogeza huduma hiyo karibu na walengwa ili kuwaondolea usumbufu wa kusafiri umbali kwenda kutoa pesa. 

Urambo ni miongoni mwa wilaya 16 ambazo ziko katika majaribio ya ulipaji walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini kwa njia ya mtandao. 

Wilaya nyingine ni Ilala, Temeke , Kinondoni, Arusha, Bagamoyo, Bahi, Kigoma, Kilwa, Kisarawe, Mkuranga, Mpanda, Muheza, Siha, Manispaa ya Songea na Unguja.

Na Tiganya Vincent, Urambo 

Share:

Leave a reply