Wazee wa Chadema watiwa mbaroni Morogoro

81
0
Share:

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linamshikilia Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Jimbo la Morogoro Kusini Mzee Daniel Banzi na Dereva wake Proaches Urassa.

Taarifa hiyo imetolewa mchana wa leo kwa umma na Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje Chadema, John Mrema ambapo amesema wanashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Morogoro.

“Jambo la kusikitisha ni kuwa jana usiku Polisi walivamia walikokuwa wamelala Viongozi na kuwakamata baadhi yao ambao ni dereva Proaches Urassa na Mzee Banzi. Hakuna maelezo ya maana yanayotolewa zaidi ya Polisi kusema ni ukaguzi wa kawaida, ila ukweli ni kwamba kila wanapoonekana viongozi wa CHADEMA Polisi wanawakamata,” amesema Mrema.

Mrema amesema Chadema inalaani kwa nguvu zote kitendo hicho kwa madai kuwa ni cha udhalilishaji dhidi ya viongozi na wanachama wa chama hicho.

Share:

Leave a reply