Waziri Kalemani akutana na wawekezaji wa teknolojia ya sumaku

250
0
Share:

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amekutana na kufanya mazungumzo na wawekezaji wenye nia ya kuzalisha umeme nchini kwa kutumia teknolojia mpya ya sumaku. Amekutana na wawekezaji hao Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma.

Baada ya kuzungumza na Waziri, wawekezaji hao kutoka Kampuni ya Tangen Investment Limited ya Ujerumani, wamefanya majadiliano na wataalam wa nishati kutoka wizarani, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA).

Wawekezaji hao wametakiwa kuwasilisha Andiko la Awali (concept note) la Mradi wao ili lipitiwe na kujadiliwa na wataalam husika, kabla ya kuendelea na hatua nyingine stahiki za uwekezaji nchini.

Share:

Leave a reply