Waziri Lukuvi agawa hati 6,000 za viwanja Kimara

503
0
Share:

Leo Agosti 7, 2017 Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi, William Lukuvi amegawa hati za umiliki za viwanja 6,000 kwenye Kata ya Kimara, Manispaa ya Ubungo.

Waziri Lukuvi mapema leo alifika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, katika ghafla ya Mradi wa Mpango Darasa iliyofanyika kwenye Kata ya Kimara, na kupokelewa na Mstahiki Meya Boniface Jacob pamoja na Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea pamoja na Watumishi wa Hamashauri.

Mradi wa Mpango Darasa ulikuwa na lengo la kuonyesha namna ya kukabiliana na Makazi holela( Squatter) katika jiji la Dar es salaam, ambapo kata mbili za Halamshauri ya manipsaa ya Ubungo zilichaguliwa na Wizara ya Ardhi kuwa sehemu ya mfano, ya Kimara na Saranga.

“Pamoja na kusuasua kwa mradi kutokana na changamoto mbalimbali,lakini leo robo ya kusudio la mradi kwa maana mitaa 3 kati ya mitaa 13,mtaa wa kirungule “A”(Hati 1458),kirungule “B” (Hati 1480) na Mavurunza (1758) Wananchi wa mitaa hiyo wamejitokeza viwanja vya Kanisa Katoliki mtaa wa kilungule “A” kwa niaba ya mitaa yote kushuhudia ugawaji wa hati 4696 za awali kabla ya mradi kifungwa rasmi,” amesema Meya Jacob

Aidha Waziri Lukuvi amewahakikishia ushirikiano Mstahiki Meya Boniface Jacob na Mbunge wa Ubungo Kubenea kuwa endapo wananchi wa sehemu zingine watahitaji Miradi kama hiyo na kuratibiwa na Halmashauri ya Ubungo,wizara ipo tayari kufanikisha miradi mingine yoyote inayoibuliwa na wananchi,badala ya kusubiria Wizara ya Ardhi peke yake.

Katika hatua nyingine, Waziri Lukuvi na Mstahiki Meya Boniface Jacob,wamekubaliana kupeleka Wizarani na Bungeni mapendekezo juu ya muundo wa ubadilishaji wa michoro na utoaji wa vibali,kuondoa kero na urasimu kwa wananchi.

Share:

Leave a reply