Waziri Mkuu mgeni rasmi mechi ya Bunge Sports Club

293
0
Share:

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mashindano yaliyoandaliwa na Bunge Sports Club kwa ajili ya kusaidia wahanga wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera, yatakayofanyika kesho katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Mechi za mpira wa miguu zitakazochezwa kesho ni pamoja na Wabunge wapenzi wa Simba na Wabunge wapenzi wa Yanga, Bongo Movie na Bongo fleva na mechi ya mpira wa pete kati ya Bunge Sports Club na TBC.

Mwenyekiti wa Bunge Sports Club amesema maandalizi ya michezo ya kesho yamekamilika na kwamba geti litaanza kufunguliwa kuanzia majira ya saa 5 asubuhi.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Alex Nkeyenge amesema tiketi zitakazotumika ni za kielekteoniki ambapo amesema kampuni ya Selcom itaweka mawakala watakaouza tiketi hizo.

Pia amesema tiketi hizo zitanunuliwa kwa njia ya mtandao wa simu kupitia M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money.

Hata hivyo, Bongo Movie na Bongo Fleva wametambiana kufunguna katika mechi yao ya kesho.

Hali kadhalika Timu ya Mpira wa Pete ya Bunge Sports Club imetamba dhidi ya TBC.

Na Regina Mkonde

Share:

Leave a reply