Waziri Mwigulu Nchemba aapishwa na kupokelewa makao makuu ya wizara

305
0
Share:

Aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mh, Mwigulu Nchemba aapishwa na kupokelewa makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi baada ya hivi karibuni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuliwa kufanya mabadiliko madogo katika Baraza lake la Mawaziri ambapo nafasi ya  Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imechukuliwa na  mbunge wa jimbo la Buchosa, Dk Charles Tizeba baada ya uteuzi wa Mheshimiwa Rais. Zifuatazo ni picha za mapokezi ya Waziri Nchemba alivyopokelewa na wafanyakazi wa wizara hiyo.

Mwigulu Nchemba na Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh, Mwigulu Nchemba (kushoto), muda mfupi baada ya Sherehe ya Kumwapisha iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.

Mwigulu na Masauni

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh, Mwigulu Nchemba(kulia), na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira(kushoto) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni, muda mfupi baada ya Rais Dkt. John Magufuli kumwapisha Waziri Mwigulu Nchemba kuongoza wizara hiyo leo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Nchemba

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mwigulu Nchemba(Kushoto), akikaribishwa Makao Makao ya Wizara hiyo na Katibu Mkuu Meja Jenerali Projest Rwegasira.Katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhandisi Hamad Masauni na wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu Balozi Yahya Simba.

Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Mawasiliano, Jane Massawe

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Mawasiliano, Jane Massawe, mara baada ya kupokelewa Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiweka saini mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, akiweka saini mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi muda mfupi baada ya kuapishwa kwake. Katikati ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Yahya Simba.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

Share:

Leave a reply