Waziri Mwijage awasili Bukoba kujionea hali ya urejeshwaji wa miundombinu Mkoani humo

226
0
Share:

Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage amewasili Mjini Bukoba alipokwenda kujionea hali ya urejeshwaji wa miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi ambapo amekutana na Kamati ya Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu.

01Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akiongea na baadhi ya Wanakamati ya Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati alipotembelea ofisi za idara hiyo leo mjini Bukoba.  Wa pili kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya

02Mkurugenzi Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Brigedia Jenerali Mbazi Msuya akifafanua jambo kwa Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles (kushoto) wakati alipomtembelea ofisini kwake leo mjini Bukoba alipokwenda kujionea hali ya urejeshwaji wa miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi.

03Waziri Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage akisaini kitabu cha wageni ofisi ya Idara ya Kuratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu wakati alipotembelea ofisi za idara hiyo leo mjini Bukoba alipokwenda kujionea hali ya urejeshwaji wa miundombinu iliyoharibiwa na tetemeko la ardhi. 

(Picha na Eleuteri Mangi, MAELEZO, Bukoba)

Share:

Leave a reply