Waziri Nape apokea Milioni 10 kutoka Skol Contractors Building Limited kusaidia waathirika wa Tetemeko Kagera

266
0
Share:

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye amepokea  kiasi cha Shilingi Milioni Kumi kutoka  Kampuni ya Skol Building  Contractors Limited.

Akipokea fedha hizo leo Jijini Dar es Salaam kutoka kwa Mwenyekiti  wa Kampuni hiyo Bw. Vincent Peter Masawe  Waziri  Nnauye amemthibitishia kuwa pesa hizo zitawasilishwa  kwa waathirika wa tetemeko hilo ili zitatue changamoto zinazowakabili.

“Ninashukuru sana kwa msaada wenu mmetambua changamoto wanazopata wenzetu,niwaombe Watanzania wote tuendelee kujitoa kuwasaidia ndugu zetu waliopata maafa haya”.Alisema Mhe.Nnauye.

pix-1-b

Mwenyekiti wa Kampuni ya Skol Building  Contractors Limited Bw.Vincent Massawe (kushoto) akikabidhi Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye(kulia) kiasi cha Shilingi Milioni Kumi taslimu leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusaidia wakazi wa Mkoa wa Kagera walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea hivi karibuni.

Aidha Mwenyekiti wa kampuni hiyo Bw.Vincent Peter Masawe amesema Kampuni yao imeguswa na matatizo waliyopata wakazi  hao wa Kagera na ndio maana  wameamua kuwasaidia ili hali zao za maisha zireje kama zamani.

“Tumeamua kuwasaidia wenzetu na tunaomba wafanyabiashara na Watanzania kwa ujumla popote walipo waguswe na jambo hili na waunge mkono Serikali katika juhudi zake za kuwasaidia waathirika wa tetemeko hili”. Aliongeza Bw.Masawe.

Katika hatua nyingine Mhe. Waziri amewakaribisha wananchi wote katika harambee ya kuchangia waathirika hao iliyoandaliwa na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) itakayofanyika Septemba 21 mwaka huu jioni katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere uliopo Jijini Dar es Salaam.

Na Shamimu Nyaki – WHUSM

pix-2

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akifurahia jambo mara baada ya kupokea msaada wa Shilingi Milioni Kumi uliotolewa na Kampuni ya SKOL Bulding Contractors Limited  Ofini kwake jijini Dar es Salaam kwa ajili ya  kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera hivi Karibuni (Kushoto) ni Bw.Vincent  Massawe kutoka Kampuni hiyo mara baada ya kukabidhi pesa hizo.

pix-3

Mwenyekiti wa Kampuni ya Skol Bulding Contractors Limited Bw.Vincent Massawe akitoa wito kwa wadau mbalimbali wa sekta binafsi kujitokeza kutoa msaada wa kuisaidia kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera alipofika ofisini kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na  Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) kumkabidhi kiasi cha Shilingi Milioni Kumi leo jijini Dar es Salaam.(Picha na Anitha Jonas – WHUSM).

Share:

Leave a reply