Waziri Nape awageukia viongozi wa mikoa

214
0
Share:

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amewaagiza wa wakuu wa mikoa na wilaya kuhakikisha  kuwa viwanja vya michezo vilivyo vamiwa  na kujengwa vina kuwa wazi ndani ya siku 30.

Nnauye  ametoa agizo hilo mkoani  Geita jana wakati akizungumza na  wasanii ,maofisa utamaduni wa mkoa, maofisa habari, wanahabari, wanamichezo, wadau wa soka  pamoja na kamati ya ulinzi na usalaama wilaya ya Geita.

Amesema kuwa  wakuu  hao wanatakiwa kuhakikisha viwanja hivyo vinakuwa wazi ndani ya siku 30 ili viwanja hivyo viweze kutumiwa na wanamichezo kwa malengo yaliyo kusudiwa  na kuibua vipaji kwa vijana na kuwataka watoe taarifa za viwanja hivyo .

”Wakuu wa mikoa na wilaya hakikisheni mnafuatilia viwanja hivyo  vina kuwa wazi ndani ya siku 30 na mnitumie taarifa kwa kila hatua,” amesema  Nnauye.

Pia amezitaka  halmashauri nchini kuwa ajiri maofisa habari pamoja na kuwapa nafasi ya kushiriki katika vikao vya maamuzi katika halmashauri zao ili waweze kutoa ushirikiano kwa waandishi wa habari ili kuepusha wanahabari kuandika habari zisizo sahihi kutokana na kutopewa ushirikiano.

 Awali kaimu mkuu wa mkoa wa Geita, Manzie  Omary Mangochie akisoma taarifa ya mkoa wa Geita amesema kuwa  mkoa huo unakabiliwa na changamoto lukuki katika sekta hiyo ikiwemo ukosefu wa viwanja vya michezo ,watalaamu wa michezo .

Alphonce     Kabilondo na  Cassimili  Mbasa ,Geita

Share:

Leave a reply