Waziri Nchemba aikataa Simba SC

221
0
Share:

Linaweza kuwa jambo la kufurahisha pale Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvivu, Mh. Mwigulu Nchemba alipovishwa mgolole na wananchi wa jimbo lake la Iramba Magharibi na kuonekana kutokufurahishwa na mgolole huo kwa sababu una rangi nyekundu.

Hayo yalitokea siku za karibuni wakati Waziri Nchemba alipotembelea jimboni kwake kwa ajili ya kuwashukuru wapiga kura wa jimbo hilo ambao walimpigia kuara na kumsaidia kurejea bungeni kwa awamu nyingine.

Sababu ya kutokufurahishwa kwake ni rangi ya mgolole huo ambao rangi yake inafanana na wapinzani wa Yanga, Simba na hivyo kuvaa kwake mlogole wenye rangi nyekundu ni kama anaishabikia Simba.

Share:

Leave a reply