Waziri Nchemba awataka wananchi kuwa na imani na Jeshi la Polisi

219
0
Share:

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka wananchi nchini kuendelea kuwa na imani kubwa na vyombo vya ulinzi na usalama nchini katika kulinda Raia na mali zao

Akizungumza nawananchi wa kata ya Kinampanda wilaya ya Iramba mkoani Singida, Waziri Mwigulu amesema kuwa kama yeye ndiye aliyepewa dhamana ya usalama wa raia na mali zao katika Wizara ya Mambo ya Ndani basi atahakikisha kunakuwa na usalama wa uhakika kwa wananchi wote bila kuwabagua.

Aidha Waziri Mwigulu amesema kuwa hata watu wanaoshambulia watu watashughulika nao mmoja mmoja hasa waliobeba jina la watu wasiojulikana, kwahiyo wananchi waendelee kuliaamini Jeshi la Polisi nchini wakati huu ambapo wanaendelea na kazi ya upelelezi wa kuwakamata watu wote waliohusika na mashambulio kwa mbunge Tundu Lissu, Afisa mstaafu wa Jeshi la Wananchi na hakimu huko Mtwara kwani uchunguzi huo auna ukomo mpaka upate wote katika idadi yao waliohusika na mashambulizi.

Waziri Mwigulu ameongeza kuwa nchi hii ni nchi huru inajitegemea hivyo hakuna haja ya vyombo vya nje vije kufanya uchunguzi, “Hawa watu wanao fanya uhalifu nchini, upelelezi utafanywa na watu wetu, watakamatwa na vyombo vyetu na watafikishwa katika vyombo vya sheria vya hapa hapa  tunatakiwa kuamini vyombo vyetu, kama serikali tutashugulikanao kweli kweli.”

Share:

Leave a reply