Waziri Prof.Mbarawa amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa ATCL

259
0
Share:

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. MAKAME MBARAWA amemsimamisha kazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), Captain Johnson Mfinanga (Pichani) na Mkurugenzi wa Uendeshaji Captain Sadick Muze kwa kosa la  kuchagua rubani mmoja ambaye hajakidhi vigezo anavyotakiwa kuwa navyo vya marubani wanaotarajia kuondoka kesho kuelekea nchini Canada kwa  ajili ya mafunzo  ya kurusha ndege mpya mbili zinazotarajiwa kuwasili nchini katikati ya mwezi Septemba.

Akizungumza na waandishi wa habari wilayani Kyela, mkoani Mbeya Prof.Mbarawa amesema baada ya kukamilisha malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mbili mpya kwa ajili ya ATCL  alitoa maelekezo kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo kuwachagua marubani watano wenye vigezo ambavyo vinahitajika kwa ajili ya mafunzo hayo jambo ambalo amebaini mmojawapo wa waliochaguliwa hajatimiza vigezo na hivyo kuamua kumsimamisha kazi kwa kosa la uzembe.

Waziri  Mbarawa amesisitiza kuwa msimamo wa serikali ni kuahakikisha kila mtumishi  wa umma anatekeleza wajibu  wake kwa kufuata sheria kanuni na taratibu hivyo atakaye kiuka msimamo huo Serikali haitasita kumchukulia hatua za kinidhamu.

Shirika la Ndege Tanzania katika mwaka huu wa fedha Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa ndege tatu.

Share:

Leave a reply