Waziri wa Fedha aipongeza Benki ya NMB kuwajali wajasiriamali wadogo

235
0
Share:

Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango ameipongeza Benki ya NMB kwa kuwajali wajasiliamali wadogo na wakati. Waziri Mpango ametoa kauli hiyo ja jijini Dar es Salaam alipokuwa akizinduwa maonesho ya mabenki na taasisi za kifedha yanayoendelea katika ukumbi wa Mlimani City.

Alisema Serikali inatambua mahitaji makubwa ya kufanya maboresho na kuziwezesha benki na taasisi nyingine za kifedha kuweza kufikia watu wengi kwa maana ya mitaji ya kutosha ya kuongeza uwekezaji wa ndani, ikiwa ni pamoja na kuweka msukumo zaidi kujenga mazingira rafiki kwa wadau wa sekta hiyo iweze kupanua huduma nchini.

Serikali inatambua changamoto anuai zinazowakabili wajasiliamali hasa wadogo na wakati hapa nchini ikiwemo kushindwa kupata mikopo kwa urahisi jambo ambalo linakwamisha mipango waliojiwekea. Aliziomba taasisi za fedha yakiwemo mabenki kubuni programu na madirisha maalumu ya kuwasaidia wajasiliamali wadogo na wakati wanaofanya jitiata kubwa kuwekeza katika viwanda vidogo.

“Napenda kuipongeza benki ya NMB kwa kuwajali wajasiliamali wadogo na wakati na hata kuamua kudhamini maonesho ya mabenki na taasisi za kifedha ili kuwakutanisha wafanyabiashara kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili. Mkusanyiko huo utachangia kuona fursa za mitaji zinazopatikana NMB pamoja na taasisi nyingine za kifedha na kuzichangamkia kwa maendeleo ya biashara zao,” alisema Waziri Mpango.

Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango (mwenye koti la kijivu) pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (wa tatu kulia) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Maonesho ya Kibenki na taasisi za fedha leo katika Ukumbi wa Mlimani City. Kushoto kwa Waziri Mpango ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya NMB, James Metairon ambao ni wadhamini wa maonesho hayo akishuhudia.

Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango (mwenye koti la kijivu) pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (wa tatu kulia) wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa Maonesho ya Kibenki na taasisi za fedha leo katika Ukumbi wa Mlimani City. Kushoto kwa Waziri Mpango ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya NMB, James Metairon ambao ni wadhamini wa maonesho hayo akishuhudia.

unnamedWaziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango akizungumza kabla ya kuzinduwa Maonesho ya Kibenki na taasisi za fedha leo katika Ukumbi wa Mlimani City.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (kushoto) akizungumza katika Maonesho ya Kibenki na taasisi za fedha akizungumza katika uzinduzi wa maonesho hayo leo katika Ukumbi wa Mlimani City.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (kushoto) akizungumza katika Maonesho ya Kibenki na taasisi za fedha akizungumza katika uzinduzi wa maonesho hayo katika Ukumbi wa Mlimani City.

unnamed-1Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya NMB, James Metairon (kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa Maonesho ya Kibenki na taasisi za fedha katika Ukumbi wa Mlimani City.

unnamed-3Mkurugenzi Uendeshaji wa Imori International, Matrina Ambrozy (kulia) akizungumza katika uzinduzi wa Maonesho ya Kibenki na taasisi za fedha katika Ukumbi wa Mlimani City.

unnamed-4Mkurugenzi wa Kikundi cha Furaha ya Wanawake Wajasiriamali kwa Viziwi Tanzania, Anneth Gerana (kushoto) akizungumza katika uzinduzi wa Maonesho ya Kibenki na taasisi za fedha katika Ukumbi wa Mlimani City.

unnamed-9Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango (mwenye koti la kijivu) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Maonesho ya Kibenki na taasisi za fedha katika Ukumbi wa Mlimani City. Kushoto kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara Benki ya NMB, James Metairon ambao ni wadhamini wa maonesho hayo akishuhudia.

unnamed-2Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji nchini, Clifford Tandari (kulia) akitembelea banda la Benki ya NMB katika Maonesho ya Mabenki na Taasisi za Kifedha yanayofanyika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

unnamed-5Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango wakiwa ndani ya banda la Benki ya NMB kwenye Maonesho ya Kibenki na taasisi za fedha akizungumza katika uzinduzi wa maonesho hayo jana katika Ukumbi wa Mlimani City.

unnamed-6Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango wakiwa ndani ya banda la Benki ya NMB kwenye Maonesho ya Kibenki na taasisi za fedha akizungumza katika uzinduzi wa maonesho hayo katika Ukumbi wa Mlimani City.

unnamed-7Baadhi ya wananchi waliotembelea Maonesho ya Kibenki na taasisi za fedha wakipata huduma ndani ya Banda la Benki ya NMB lililokuwa likifungua akaunti za Chap Chap kwenye uzinduzi wa maonesho hayo katika Ukumbi wa Mlimani City.

unnamed-8Baadhi ya Wajasiriamali wenye ulemavu wa kusikia wakionesha bidhaa zao kwenye maonesho hayo.

Share:

Leave a reply