West Ham United yagoma kumwachia Dimitri Payet

463
0
Share:

Licha ya kiungo wa West Ham United, Dimitri Payet kuomba uongozi wa klabu hiyo kumwachia kuhamia timu nyingine, uongozi wa timu hiyo unaonekana kuweka ngumu kumwachia Payet kwani bado inahitaji kumtumia kwa muda mrefu zaidi.

Kocha wa Wes Ham, Slaven Bilic amethibitisha kuwa Payet anataka kuihama klabu hiyo kwenda kucheza timu kubwa zenye mafanikio lakini uongozi wa klabu hiyo upo tayari kumpa kila kitu ili kuhakikisha anasalia katika klabu hiyo ambayo anamkataba nayo mpaka 2021.

“Tuna shida na mchezaji wetu Payet, anataka kuondoka, tulishasema hatutauza wachezaji wetu muhimu lakini Payet hataki kucheza kwetu, hatutamuuza. Hii timu, uongozi, tunampa kila kitu, tupo kwa ajili yake,” amesema Bilic.

Aidha baadhi ya vilabu tayari vimeanza kuonyesha nia ya kutaka kumsajili ikiwepo Paris Saint-German, klabu yake ya zamani Marseille na baadhi ya timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya China.

Share:

Leave a reply