Wilshere aweka picha ya wakongwe wa Man Utd mtandaoni, mashabiki wamshambulia kwa maneno

223
0
Share:

Linaweza likawa sio jambo la kawaida hasa kutokana na upinzani uliopo baina ya vilabu vya Manchester United na Arsenal ambapo baada ya mchezo wa Arsenal na Crystal Palace, mchezaji wa Arsenal,  Jack Wilshere aliweka picha katika akaunti yake ya Facebook iliyo na maneno yaliyosomeka “THIS IS OUR CLUB TODAY AND FOREVER”.

2016-04-19

Picha aliyoiweka Wilshere katika akaunti yake ya Facebook.

Lakini chini ya picha hiyo kukiwa na picha ya wakongwe wa Manchester United Bobby Charlton, George Best na Denis Law ambao waliisaidia Man United kushinda kombe la European Cup mwaka 1968 na picha hiyo ni sanamu ambalo lipo katika Uwanja wa Man United, Old Trafford.

Baada ya kuweka picha hiyo mashabikiwa Manchester United wakaanza kumwekea maoni yao kutokana na kuona Wilshere kaweka picha ya kuzungumzia Arsenal na chini ikiwa na picha ya wachezaji wa zamani wa Manchester United.

Alex Day: Haven’t you taken this down yet you retard?

Kurt Smith: haha ALWAYS in our shadow

Sonnie Adjus: Fake gunners

Adi Juris S. Ali: It’s hopeless to depend on someone even he’s the Professor or star rated player, i just believe on this team to be better than perfect in every match. Hope is useless, but football is some kind of spirit. That’s why l’ve left united fans 4 years ago for this team.#COYG  

Share:

Leave a reply