Wizara ya Afya yahamia Dodoma rasmi, yaanza na Mawaziri wake na Watendaji Wakuu

2592
0
Share:

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, tayari imechukua hatua ya kutekeleza agizo la Rais wa Serikali ya awamu ya tano ya kuhamia  makao makuu ya nchi  Mjini Dodoma, ambapo kuanzia juzi na jana Wizara hiyo imeweza kuhamishia vitu vyake mkoani Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kitengo cha Habari Wizara ya Afya, imetoa taarifa ya kuufahamisha Umma kuwa, Awamu ya Kwanza ya Watumishi wa Wizara kuhamia Makao Makuu ya Nchi, Mkoani Dodoma imetekelezwa tarehe 23 Februari, 2017.

Taarifa hiyo imeweka wazi kuwa, Miongoni mwa waliohamia Dodoma katika awamu hii ya kwanza ni pamoja na Viongozi na Watendaji Wakuu wa Wizara wakiongozwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy A. Mwalimu, Naibu Waziri Mhe. Dkt.Hamisi Kigwangalla, pamoja na Makatibu Wakuu wa Wizara Idara kuu ya Afya na Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.

Kufuatia Uhamisho huo, jumla ya watumishi 90 wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wameungana na viongozi wao kuitikia uhamisho huo.

Kufuatia kuhamia Dodoma, kwa sasa  Anwani za Wizara zitakazotumika mkoani Dodoma  kwa shughuli zote za kiofisi ni:

Katibu Mkuu,

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,

Idara Kuu ya Afya,  

Chuo Kikuu Dodoma,

Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii,

S.L.P 743,

Jengo Namba 11,

DODOMA.

Namba ya Simu +255 26 2323267

Katibu Mkuu,

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,

Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,

Chuo Kikuu Dodoma,

Kitivo cha Sanaa na Sayansi ya Maendeleo ya Jamii,

S.L.P 573,

Jengo Namba 11

DODOMA.

Baadhi ya vitu vikishushwa mjini Dodoma vikitokea Jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya vitu vikishushwa mjini Dodoma vikitokea Jijini Dar es Salaam. Tayari Wizara ya Afya imeanza kuhamia Makao Makuu ya nchi.

Share:

Leave a reply