Wizara ya Afya yatoa takwimu ya vifo vitokanavyo na Magonjwa yasiyo ya kuambukiza

769
0
Share:

Watanzania wametakiwa kufanya mazoezi ya mwili na kuacha tabia ya mazoe hasa yale ya unywaji wa pombe wa kupitiliza, uvutaji wa sigara na kula vyakula visivyofuata mpangilio ili kuepuka magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo yamekuwa yakisababisha vifo vingi nchini na Duniani kwa ujumla.

Ambapo ili kuepuka hilo, wametakiwa kufanya mazoezi ya mara kwa mara ya viungo ili kujenga Afya njema na mwili kupambana na magonjwa nyemelezi.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa magonjwa yasioambukiza (NCD) Prof. Ayoub Magimba mapema leo 9 Januari 2017 Jijini Dar es Salaam ambapo ameeleza kwa undani juu ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza au magonjwa sugu, (kwa lugha ya kigeni hujulikana kama Non Communicable Diseases au Chronic Diseases).

Akifafanua hilo, Prof. Magimba amesema magonjwa ambayo mtu akiyapata hawezi kumwambukiza mwingine na ataishi nayo hadi siku ya kufa, yamekuwa yakiongezeka sana duniani kote, haswa kwenye nchi zilizo chini ya Jangwa la Sahara, Tanzania ikiwemo huku yakichangia asilimia 27, ya vifo vyote duniani.

“Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni pamoja na saratani, magonjwa ya moyo, magonjwa sugu ya njia ya hewa , seli mundu (sickle cell disease), magonjwa ya akili na dawa za kulevya, magonjwa ya figo, kisukari, ajari  , na magonjwa ya macho”. Alieleza  Prof. Magimba

Imeelezwa kuwa, mwaka 2005, katika vifo million  58 vilivyotokea duniani, vifo milioni 35 vilitokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza (NCDs).  Kwa Tanzania, utafiti uliofanyika katika wilaya nne kuanzia mwaka 1994-2002, ulionyesha kuwa asilimia 18-24 ya vifo vilivyotokea vilitokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

Moja ya vileo ambavyo vimekuwa  vikiongeza hali  kubwa ya magonjwa yasiyoambukiza

“WHO walikadiria kuwa asilimia 20, ya vifo vyote vilivyotokea hapa nchini mwaka 2005 vilitokana na magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Huku  magonjwanjwa ya moyo asilimia 9,saratani asilimia 4,magonjwa ya mfumo wa hewa asilimia 2, kisukari asilimia 1, na magonjwa mengine sugu asilimia 4.

Utafiti wa viashiria vya magonjwa yasiyo ya kuambukiza uliofanywa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) mwaka 2012, ulionyesha kuwa kuna ongezeko kubwa la viashiria vinavyosababisha magonjwa yasiyo ya kuambukiza” alieleza Prof. Magimba.

Kwa upande wa suala la Utafiti mwingine, asilimia 15.9, ya wananchi wanavuta sigara, asilimia 29.3, wanakunywa pombe, asilimia 97.2, wanakula mboga mboga na matunda chini ya mara tano kwa siku.

Aidha utafiti ulionyesha asilimia 26, ya wananchi ni wanene kupita kiasi, asilimia 26, wana lehemu nyingi mwilini, asilimia 33.8, wana mafuta mengi mwilini, asilimia 9.1, wana kisukari na asilimia 25.9, wana shinikizo kubwa la damu.

Mkurugenzi Msaidizi wa magonjwa yasioambukiza (NCD) Prof. Ayoub Magimba akizungumza mapema leo 9 Januari 2017 Jijini Dar es Salaam

Utafiti pia ulionyesha robo ya wananchi waliohojiwa hawajishughulishi na kazi za nguvu na hawafanyi mazoezi yeyote.

Hata hivyo, Prof. Magimba amesema kuwa, Magonjwa yasiyo ya kuambukiza na ya akili yamekuwa yakiongezeka sana duniani na hata hapa nchini huku takwimu  zikionyesha tatizo kuwa la Kimataifa (global growing problem). huku yakisababisha vifo milioni 36 duniani ambayo ni sawa na asilimia 63 ya vifo milioni 57 vilivyotokea duniani mwaka 2008.

Katika magonjwa hayo, Saratani ni kati ya magonjwa saba yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya watu wazima hapa nchini. Inakadiriwa kuwa wastani wa wagonjwa 109 hugundulika na saratani kila sika hapa nchini Tanzania, na asilimia 82,  ya vifo husababishwa na saratani. Hii ina maana ni asilimia 6 ya vifo vyote kwa siku hutokana na saratani.

Mkurugenzi Msaidizi wa magonjwa yasioambukiza (NCD) Prof. Ayoub Magimba akionyesha moja ya nakala ya mpango wa wizara hiyo juu ya kupambana na magojwa yasiyo ya kuambukiza mapema leo 9 Januari 2017 Jijini Dar es Salaam.

Share:

Leave a reply