Wizara ya Afya yatoa ufafanuzi juu ya wanafunzi wa NACTE

856
0
Share:

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia kwa Mkuu wake wa  kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya Bw. Nsachris Mwamwaja (Pichani kushoto) wametoa ufafanuzi  juu ya taarifa zilizokuwa zimezagaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na wanafunzi ambao walitakiwa kuendelea na mafunzo ngazi nyingine baada ya kufaulu mitihani yao, na kuchelea kuendelea na hatua nyingine kwa kuwa majibu ya mitihani yao yalikuwa hayajatoka.

“ Wizara ya Afya inapenda kutoa ufafanuzi kufuatia barua  ya mwezi Novemba, 2016 iliyotumwa kwenda kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na ambayo inazunguka kwenye mitandao ya kijamii.

Lengo la barua hiyo lilikuwa ni kutoa ushauri kwa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi  (NACTE) juu ya wanafunzi ambao walitakiwa kuendelea na mafunzo ngazi nyingine baada ya kufaulu mitihani yao, na kuchelea kuendelea na hatua nyingine kwa kuwa majibu ya mitihani yao yalikuwa hayajatoka”.

Mwamwaja  amebainisha kuwa, Kupitia taarifa hii wangependa kuwataarifu kwamba mitihani ya wanafunzi hao imeanza kusahihishwa toka tarehe 5 Desemba 2016. Hivyo, ushauri uliotolewa katika barua ile kwa sasa utakuwa umepitwa na wakati na majibu ya mitihani hiyo yanatarajiwa kutoka katikati ya mwezi Januari 2017.

Aidha vyeti vya wahitimu wa marudio “supplementary” na wa mwezi April orodha na matokeo yao yaliwasilishwa NACTE  kwa ajili ya utayarishaji wa vyeti. ilieleza Mwamwaja.

 

Share:

Leave a reply