Wizara ya Maliasili na UNDP wakubaliana kuanzisha kikosi kazi cha pamoja

164
0
Share:

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (MB) amekutana na kufanya mazungumzo Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa (UNDP) nchini Bi. Natalie Boucly katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo ya Maliasili na Utalii iliyopo Mpingo House Jijini Dar es Salaam.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Dk. Kigwangalla amekubaliana na Mkurugenzi huyo mkazi wa UNDP kuanzisha kikosi kazi cha pamoja kati ya wizara yake na UNDP kuhusiana na utafiti juu ya tuhuma zilizotolewa na kituo cha ITV London kuhusu suala la ujangili wa tembo kwenye hifadhi ya Taifa ya Ruaha, iliyopo mkoani Iringa.

Mbali na hilo Waziri Dk. Kigwangalla alimwakikishia kuwa Wizara yake ipo katika kuongeza watalii nchini kwa kutumia mbinu mbalimbali zikiwemo za kuwashirikisha wananchi ikiwemo kuandaa mwezi wa Urithi wa Tanzania, pia suala la mfumo wa malipo ya kielektroniki katika maeneo mbalimbali ya Utalii.

Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla akifurahi jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa (UNDP) nchini Bi. Natalie Boucly baada ya kumaliza kufanya mazungumzo katika ofisi ndogo ya Wizara hiyo ya Maliasili na Utalii iliyopo Mpingo House Jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo alishukuru kukutana na Waziri Dk.Kigwangalla ambapo pia amemuakikishia kuendeleza ushirikiano katika mambo mbalimbali ya kuendeleza Utalii nchini pamoja na mausuala ya Utalii.

Pia Mkurugenzi huyo amemwakikishia kusaidiana nae kwenye masuala ya uhifadhi wa misitu, wanyamapori, pamoja na kuendeleza Utalii Nchini Tanzania.

Share:

Leave a reply