Yusuph Kikwete afanya uzinduzi wa barbershop ya kwanza Bagamoyo

364
0
Share:

Kwa miaka mingi mji wa Bagamoyo uliopo mkoa wa Pwani umeonekana kuwa nyuma na wengi wakidai kuwa huo ni mji wa kihistoria hivyo ni vyema ukiwa katika mwonekano wa kihistoria ili kuwavutia watalii zaidi kutoka nje ya nchi.

Lakini kwa sasa jambo hilo limepitwa na Bagamoyo inaanza kuwa katika mwonekano wa kuvutia na katika kuendeleza jambo hilo, kwa mara ya kwanza katika historia ya mji huo, Bagamoyo imepata saluni iliyo na hadhi kwa kutoa huduma nyingi na bora (barbershop) ambayo imepewa jina la Middle Star.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni kaka wa Rais wa Tanzania wa awamu ya nne, Yusuph Kikwete ambaye pamoja na kufanya uzinduzi huo pia aliupongeza uongozi wa barbershop ya Middle Star kwa kufanya mji wa Bagamoyo kuwa na mwonekano wa kisasa kwa kupata saluni yenye hadhi kubwa.

Yusuph

Mgeni rasmi katika uzinduzi wa barbershop ya Middle Star, Yusuph Kikwete akizungumza na Mkuu wa Idara ya Habari na Masoko wa Middle Star, James Mbuligwe kuhusu huduma ambazo amezipata Middle Star Barbershop.

“Huduma hizi tulikuwa hatujawahi kuzipata hapa Bagamoyo ilikuwa mpaka uende Dar ndiyo unazipata kwahiyo mimi niwapongeze sana kwa jambo hili naamini kuanzia sasa hata Mkuu wa wilaya atakuwa anakuja hapa maana mimi mwenyewe nimepata huduma na nimeona jinsi zilivyo bora,” alisema Kikwete.

Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Habari na Masoko wa Middle Star, James Mbuligwe alisema pamoja na uwekezaji ambao wameufanya sasa, bado wamejipanga kuboresha huduma wanazozitoa ili kuifanya saloni hiyo kuwa na hadhi kubwa zaidi jambo ambalo litawezesha hata wageni wa kitaifa wanaofika wilayani hapo kushawishika kutumia saluni hiyo.

DSC_0290

Mkuu wa Idara ya Habari na Masoko wa Middle Star, James Mbuligwe akielezea kuhusu saluni hiyo na jinsi ambavyo wamejipanga kuboresha huduma zao. Kushoto ni Kaimu Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bagamoyo, Salumu Mtelela.

“Kwa sasa tumeanza lakini bado kuna mambo hivi karibuni tutaongeza na mojawapo tunatakuwa kuwa na chumba cha VIP na hicho kitakuwa kikihusika na watu maalum ambao wanafika hapa kupata huduma kwa hakika tunataka kuhakikisha tunatoa huduma bora ambazo hazikuwahi kuwa zikitolewa awali,” alisema Mbuligwe.

DSC_0250

Mgeni rasmi katika uzinduzi, Yusuph Kikwete akipatiwa huduma.

DSC_0267

DSC_0278

Kaimu Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bagamoyo, Salumu Mtelela akipatiwa huduma.

DSC_0299

Mgeni rasmi Yusph Kikwete akiwa kattika picha ya pamoja na Kaimu Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Bagamoyo, Salumu Mtelela, Mkuu wa Idara ya Habari na Masoko wa Middle Star, James Mbuligwe na wafanyakazi wengine wa saluni hiyo katika picha ya pamoja.

Share:

Leave a reply